ULIMWENGU WA MAWASILIANO TOKA TZ

Friday, July 22, 2011

NIMEKUJA BONGO KUWASHIKA


Msanii mkali wa hip hop kutoka nchini Kenya Ramadhani chambo anaejulikana kwa jina la Sharama amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa albamu yake ya vunja winga hapa Tanzania kutokana na kuona ana mashabiki wengi hapa nchini halaf hawajapata kile wanachostahili kutoka kwake
Akizungumza na mwandishi wetu Sharama alikuwa na haya ya kusema “unajua nilikaa na kuona kuwa watanzania ni miongoni mwa mashabiki wangu na ninawapenda sana ndio maana nimeamua kiuja kuwapa kile wanachokihitaji kutoka kwangu”
Sharama ambae kwa sasa yupo hapa bongo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka katika lile kundi la Ukoo Flani Maumau wote kwa pamoja wakiwa wamepiga kambi pale katika studio za Mzuka Record wakipata madini tofauti kutoka kwa mtu mzima Benjamini wa mambojambo
Aliendelea sharama kwa kuwaomba mashabiki wake wote kuhudhuria kwa wingi pale Diamond jubilee siku ya tarehe 23/07 ambapo ndipo atakuwa akizindua albamu yake ya VUNJA WINGA. “mimi ninachowaomba mashabiki wangu wa Tanzania ni kuibuka kwa wingi pale Diamond ili kuona nimewaandalia nini kama zawadi yao maana nina imani kuwa kuna kitu kikubwa mashabiki wangu wanakihitaji kutoka kwangu hivyo na mimi nitawapa siku hiyo”
Sharama pia ameishukuru taasisi isiyo ya kiserikali ya Art In Tanzania kwa kuwezesha mpango mzima wa uzinduzi wake.
Katika uzinduzi huu pia kutakuwa na uzinduzi wa albamu ya HAIELEWEKI yak wake Totoo ze bingwa ambao nao kwa kiasi kikubwa umewezeshwa na kuletwa kwenu na Art In Tanzania
Katika shoo hii watu wazima hawa watasindikizwa na kundi zima la ukoo flani maumau, Abasi kutoka nchini Kenya na kutoka tanzanina watakuwepo 20%, Benjamini wa mambojambo, Zolla D, Sana asana Band na bendi ya Akudo Impact.

WATEULE TOUR IN SOUTH AFRICA with Dj Choka Friday, July 22, 2011

                                                                
Show zinaanza rasmi Jumamosi hii ya tarehe 23 pale Joburg halafu Jumapili ya tarehe 24 tutaelekea Pretoria, baada ya hapo wiki ijayo Jumamosi ya tarehe 30 tutakuwa Cape Town kwenye Vunja Jungu na kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Tunawakaribisha watanzania wote pamoja na marafiki zetu wa huku huku South kuja kuona show nzuri kutoka bongo.

Bongo Radio and FunkHouse Entertainment did their annual party in Chicago which included the performances by Wakazi and Gwaii, and also a Fashion Show by African Models, showing coutures of one of the local Chicago designers. Prior to the evening event, people enjoyed a "barbeque at the beach" event where everyone met and enjoyed the free treatment provided by the orginizers. Be on the Look out for the Video of the performance



Thursday, May 26, 2011


WASANII WA BONGO FREVA NDANI YA MAISHA CLUB DAR ES-SALAAM 

Sam wa Ukweli



                                                                        TMK Family
                                                                            Allykiba




Tuesday, May 24, 2011

                                  
             Bonta kuzindua ulbum may 27 Morogoro    
                                                                              


 Mkali toka River Camp Soldiers,Bonta atazindua album yake ya Kila ki2 Nyerere,Ijumaa ya tarehe 27 May,2011 pande za 4 Star Club mkoani Morogoro

Hip-Hoper Joh Makini,G-Nako,Nick wa Pili,artist toka THT,PiPi na Hussein Machozi wamepata shavu la kupiga show ya uzinduzi wa album ya Kila Ki2 Nyerere ya Bonta....!



Monday, May 23, 2011

                          Mwanadada ambae ni raper kutoka nchini marekani Miss Eriott

Sunday, May 22, 2011


                                          smart boy na mshikaji flani toka misifas camp
                                   Duly on the stage VIP Club ndani ya usiku wa kiduku

                                                 duly akicheki mafans wke ndani ya VIP

baada ya interview na jstar & k-pesa mbili kilichofata ni pic kabla ya kuelekea VIP club kwa ajiri ya show

Hapa ndani ya show ya Surturday Club ya jstar ndani ya Nuru Fm Radio, smart boy nae alipata wasaa wa kumuuliza duly swali la kizushi pia raaaaaaaaaaaaaaaa!

Saturday, May 14, 2011

Watangazaji wa Radio Nuru Fm mkoani iringa kushoto ni Shani Mwenda na Zulfa Shomary 

Mtu mzima jstar na Shani Mwenda katika pozi nje ya Radio 

Saturday, March 5, 2011

Yule Pale by Redsan

C.M.B. Prezzo ft A.Y. - Nipe Nikupe

AY binadamu

NEW TRACK: SHEMEJI YENU "BABA LEVO"


Masanii wa bongo freva Tanzania anae fahamika kwa jina CLAYTON REVOCATUS a.k.a BABA LEVO ambae pia ni member wa  kundi la TMK wanaume halisi ameachia ngoma mpya ianyokwenda kwa jina SHEMEJI YENU.

wimbo huu umetengenezwa kwenye
 studio za JALA MAN REC zilizopo M nyamala jijini Dar es Salaam Tanzania.

baba levo amesema ameamua  kuitambulisha ngoma hii, baada ya ngoma yake u
inayokwenda kwa jina la SHOSTY NEY kuzuiliwa studio na
 uongozi wa jala man rec, kwa madai eti nimemdis sana Ney wa mitego.


amesema kuwa kwa vile Ngamia haelemewi na nundu yake  ameamua kuachia jiwe lingine linalokwenda kwa jina la SHEMEJI YENU naamini ngoma ni kali ila wewe pia unayo
nafasi ya kutoa maoni yako mzazi.

“UMECHAKACHUA”-OCHU


Tangu neno ‘chakachua” liingie mtaani na kushika chati hapa nchini, limekuwa likitumika kuelezea takribani kila kitu ambacho hakiendi sawa.
Ilikuwa ni suala la kusubiri tu kabla ya msanii fulani hajalitumia neno hilo katika wimbo au kuupa wimbo jina hilo.
Naam, hakuna haja ya kuendelea kusubiri kwani yupo msanii mpya ambaye ameamua kuingia na wimbo unaokwenda kwa jina hilo.
Msanii huyu mpya anaitwa Ochu Eddy Sheggy.Yes,ni mtoto wa Marehemu Eddy Sheggy, yule mwimbaji mahiri wa muziki wa dansi aliyewahi kutamba sana.
Wimbo huu umetengenezwa katika studio mpya za Seductive Records chini ya Producer Jilly Baby.
Na Video ya wimbo huu ambayo tayari imeshaanza kusambazwa katika vituo mbalimbali vya TV imetengenezwa na EmptySoulz Production.

Bongo Flava meets Brooklyn Flava, featuring Mzungu Kichaa (DK/TZ), Fid Q (TZ) & Okai (NY)



Mustafa Hassanali’
Leo march  4 na kesho march 5, mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali’ atazindua rasmi toleo lake la kiafrika, katika onyesho kubwa na la aina yake la Mmma MIA, linaloletwa kwenu kwa hisani ya utepe mweupe nchini na ‘Vodacom foundation’.

Onyesho hilo la Mmma MIA lenye lengo la kuchangia na kuhamasisha suala zima la uzazi salama nchini, litafanyika kwa siku mbili mfululizo, toka Ijumaa katika Hoteli ya Movenpick na viwanja vya Mnazi Mmoja kwa siku ya Jumamosi tarehe 5.

Onyesho hilo limepewa jina la ‘Mmma MIA’ kutokana  na sherehe za  miaka mia moja ya siku ya wanawake duniani, na miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania , kwa madhumuni ya kuhamasisha uzazi salama nchini, na kuzindua rasmi toleo jipya la Mustafa Hassanali.

Akiongea kuhusu maandalizi, Muandaaji wa maonyesho hayo la Mamma MIA, Mustafa Hassanali amesema “tuko katika maandalizi ya mwisho  ya onyesho, wageni wetu wabunifu toka nje wameshawasili nchini, na tuko tayari kuwasilisha ubunifu wetu kwa watanzania wapenda ubunifu wa mavazi, na jamii kwa ujumla”

Wabunifu waalikwa ambao wanatarajiwa kuonyesha ubunifu wao siku hiyo, mbali na Mustafa Hassanali, ni Farouque Abdella toka Zanzibar , Minna Hepburn toka Finland na Henrietta Ludgate toka Uingereza, ambapo wao wamezindua mavazi yao katika maonyesho yaliokwisha hivi karibuni ya ‘London Fashion Week’.

Monday, February 21, 2011

moja ya mastaa wa kibongo

Sagini Majura





 watangazaji wa Nuru Fm Edward Sagini Majura na Shany Mwenga ndani ya studio za Nuru Fn.


 mamito akiwa na pozi za harusi



 dullayo katika pozi

 N2N Army in da house



 moja ya mafansi wa Nuru Fm katikati ni Fady Ze Utamu



Binadamu hawezi lakini mbwa anaweza

utadhani maandamano kumbe wanavuka kutoka Kigamboni hadi Ferry a.k.a Posta


usafiri wa boti wa mv Magogoni ni moja ya kitega uchumi kikubwa na msaada mkubwa wa wanadar es salaam na watu wengine, kinachowawezesha kuvuka kutoka Posta hadi Kigambmboni au kutoka Kigamboni hadi Posta.

ajari mbaya

baadi ya ajari duniani zinavyo gharimu maisha ya watu, jamaa alikuwa ni dereva pikipiki akiwa amekatika na kugawika vipande viwili baada ya kugongano uso kwa uso na gari.

Wednesday, February 16, 2011

utazani amelewa kumbe hanywi yeye

moja ya wafanyakazi wa Nuru Fm mkoani Iringa, wakwanza ni paulina & Beatrice

Tuesday, February 15, 2011

moja ya mastaa wanaotumia gharama kubwa katika mavazi na kujilemba






jamaa noma ila tukumbuke HIV

unaweza kusema ni raha kwa namna hii ila tukumbuke kuwa vifo vingi husababishwa kwa namna hii ya kujamiana bila kutumia njia sahii nikimaanisha kutumia kinga,Tanzania tujichunge.

KUTOKA UPRESENTER HADI DJ, BONGE MOJA LA SKILLS


HIZI NI NGUVU ZA WATU NA SISI TUJARIBU

hizi ni moja ya studio kali zinazohitajika katika music production industries, japo gharama ni kubwa tujitahidi kujibana na kufanikisha tunakuwa na studio za kisasa na kufanya miziki wa bongo ukafika mbali, mfano halisi ni katika Tamasha lililoisha hivi karibuni kule visiwani zanzibar, kwa baadhi ya vikundi vya Tanzania kufanya vibaya katika Tamasha hilo.

moja ya rangi zilizotamba siku ya tarehe 14 ya mwezi huu

kudadadeki hii ndio ilikuwa bonge moja la staili ya Valentine day siku ya jana nilijaribu kuchunguza kuanzia uvaaji hadi utokaji wa baadhi ya watu nikagundua kuwa huyu dada alitisha ile mbaya kutoka nyanda za juu kusini Mkoani Iringa, kwa jinsi alivyoulemba mdomo tu no discution kwa hilo.

naomi kipangura moja ya mapresenter machachali wanaokuja kwa nguvu ya ajabu katika pozi la valentine

vipaji kama hivi havifai kupotezwa na kuviacha vikiteketa wadau, mnatakiwa kuvifata vipaji vilipo na si kusubili vije  anaitwa naomi kipangula, ambae kwa sasa anatarajia kuhitimu elimu ya uandishi wa habari mwezi juni mwaka huu, kutoka Royal college of Tanzania pande za Town ya juu Dar es Salaam, Tz.

yap hili ndo chama

moja ya kundi lililosumbua sana Royal college of Tanzania.

Sunday, February 13, 2011

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA BUSU KWA MARA YA KWANZA




Jemma Benjamin msichana mwenye umri wa miaka 18 alikuwa kwenye matembezi  na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 21, mwanafunzi wa chuo kikuu, Daniel Ross.

Mwisho wa matembezi yao, kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao wa miezi mitatu, Daniel alimpiga busu Jemma ambaye ghafla baada ya busu hilo alijinyoosha kwenye kiti huku akitoka mapovu mdomoni na kufariki hapo hapo mbele ya mpenzi wake.

Kwa mujibu uchunguzi wa Nuru Fm kupitia mitandao mbalimbali, Jemma alifariki kutokana na ugonjwa wa kifo cha ghafla (Sudden Adult Death Syndrome) ambao hupelekea vifo vya watu 500 kila mwaka nchini Uingereza.

Daniel aliwaambia polisi kuwa kwa mara ya kwanza katika uhusiano wake wa miezi mitatu na Jemma, siku hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpiga busu mdomoni.

Akielezea kifo cha mpenzi wake, Daniel amesema kuwa Jemma alifunga macho yake, alianza kutokwa na mapovu mdomoni alijinyoosha kwenye kiti na kufariki dunia.

Familia ya Jemma imesema kuwa imeshtushwa na kifo cha ghafla cha binti yao kwani alikuwa mwenye afya njema na mchezaji  mzuri wa mpira wa magongo.


MWISHO

Pata info za Dogo Janja toka Kilimanjaro

moja ya wasanii wadogo na machachari na wenye mashairi ya kuwatisha wakongwe katika gemu ya bongo freva nchini Tanzania, anaitwa Dogo janja toka kaskazini pande za A-Tawn kijenge juu, lakini kwa sasa licha ya kujipatia mshiko kwa njia hiyo pia ni mwanafunzi wa kidacho cha kwanza katika shule ya Makongo Secondary School iliyopo jijini Dar es Salaam