ULIMWENGU WA MAWASILIANO TOKA TZ

Saturday, March 5, 2011

Yule Pale by Redsan

C.M.B. Prezzo ft A.Y. - Nipe Nikupe

AY binadamu

NEW TRACK: SHEMEJI YENU "BABA LEVO"


Masanii wa bongo freva Tanzania anae fahamika kwa jina CLAYTON REVOCATUS a.k.a BABA LEVO ambae pia ni member wa  kundi la TMK wanaume halisi ameachia ngoma mpya ianyokwenda kwa jina SHEMEJI YENU.

wimbo huu umetengenezwa kwenye
 studio za JALA MAN REC zilizopo M nyamala jijini Dar es Salaam Tanzania.

baba levo amesema ameamua  kuitambulisha ngoma hii, baada ya ngoma yake u
inayokwenda kwa jina la SHOSTY NEY kuzuiliwa studio na
 uongozi wa jala man rec, kwa madai eti nimemdis sana Ney wa mitego.


amesema kuwa kwa vile Ngamia haelemewi na nundu yake  ameamua kuachia jiwe lingine linalokwenda kwa jina la SHEMEJI YENU naamini ngoma ni kali ila wewe pia unayo
nafasi ya kutoa maoni yako mzazi.

“UMECHAKACHUA”-OCHU


Tangu neno ‘chakachua” liingie mtaani na kushika chati hapa nchini, limekuwa likitumika kuelezea takribani kila kitu ambacho hakiendi sawa.
Ilikuwa ni suala la kusubiri tu kabla ya msanii fulani hajalitumia neno hilo katika wimbo au kuupa wimbo jina hilo.
Naam, hakuna haja ya kuendelea kusubiri kwani yupo msanii mpya ambaye ameamua kuingia na wimbo unaokwenda kwa jina hilo.
Msanii huyu mpya anaitwa Ochu Eddy Sheggy.Yes,ni mtoto wa Marehemu Eddy Sheggy, yule mwimbaji mahiri wa muziki wa dansi aliyewahi kutamba sana.
Wimbo huu umetengenezwa katika studio mpya za Seductive Records chini ya Producer Jilly Baby.
Na Video ya wimbo huu ambayo tayari imeshaanza kusambazwa katika vituo mbalimbali vya TV imetengenezwa na EmptySoulz Production.

Bongo Flava meets Brooklyn Flava, featuring Mzungu Kichaa (DK/TZ), Fid Q (TZ) & Okai (NY)



Mustafa Hassanali’
Leo march  4 na kesho march 5, mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali’ atazindua rasmi toleo lake la kiafrika, katika onyesho kubwa na la aina yake la Mmma MIA, linaloletwa kwenu kwa hisani ya utepe mweupe nchini na ‘Vodacom foundation’.

Onyesho hilo la Mmma MIA lenye lengo la kuchangia na kuhamasisha suala zima la uzazi salama nchini, litafanyika kwa siku mbili mfululizo, toka Ijumaa katika Hoteli ya Movenpick na viwanja vya Mnazi Mmoja kwa siku ya Jumamosi tarehe 5.

Onyesho hilo limepewa jina la ‘Mmma MIA’ kutokana  na sherehe za  miaka mia moja ya siku ya wanawake duniani, na miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania , kwa madhumuni ya kuhamasisha uzazi salama nchini, na kuzindua rasmi toleo jipya la Mustafa Hassanali.

Akiongea kuhusu maandalizi, Muandaaji wa maonyesho hayo la Mamma MIA, Mustafa Hassanali amesema “tuko katika maandalizi ya mwisho  ya onyesho, wageni wetu wabunifu toka nje wameshawasili nchini, na tuko tayari kuwasilisha ubunifu wetu kwa watanzania wapenda ubunifu wa mavazi, na jamii kwa ujumla”

Wabunifu waalikwa ambao wanatarajiwa kuonyesha ubunifu wao siku hiyo, mbali na Mustafa Hassanali, ni Farouque Abdella toka Zanzibar , Minna Hepburn toka Finland na Henrietta Ludgate toka Uingereza, ambapo wao wamezindua mavazi yao katika maonyesho yaliokwisha hivi karibuni ya ‘London Fashion Week’.