ULIMWENGU WA MAWASILIANO TOKA TZ

Sunday, February 13, 2011

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA BUSU KWA MARA YA KWANZA




Jemma Benjamin msichana mwenye umri wa miaka 18 alikuwa kwenye matembezi  na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 21, mwanafunzi wa chuo kikuu, Daniel Ross.

Mwisho wa matembezi yao, kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao wa miezi mitatu, Daniel alimpiga busu Jemma ambaye ghafla baada ya busu hilo alijinyoosha kwenye kiti huku akitoka mapovu mdomoni na kufariki hapo hapo mbele ya mpenzi wake.

Kwa mujibu uchunguzi wa Nuru Fm kupitia mitandao mbalimbali, Jemma alifariki kutokana na ugonjwa wa kifo cha ghafla (Sudden Adult Death Syndrome) ambao hupelekea vifo vya watu 500 kila mwaka nchini Uingereza.

Daniel aliwaambia polisi kuwa kwa mara ya kwanza katika uhusiano wake wa miezi mitatu na Jemma, siku hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpiga busu mdomoni.

Akielezea kifo cha mpenzi wake, Daniel amesema kuwa Jemma alifunga macho yake, alianza kutokwa na mapovu mdomoni alijinyoosha kwenye kiti na kufariki dunia.

Familia ya Jemma imesema kuwa imeshtushwa na kifo cha ghafla cha binti yao kwani alikuwa mwenye afya njema na mchezaji  mzuri wa mpira wa magongo.


MWISHO

No comments:

Post a Comment